Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » Amchana Mwanaye kwa Wembe aweze kujisaidia.....Mtoto huyo alizaliwa bila kuwa na sehemu ya haja kubwa


Mkazi wa Kata ya Kitangiri katika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, Anastazia Ngilitu, amemchana kwa wembe mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili na wiki mbili baada ya mtoto huyo kuzaliwa bila kuwa na sehemu ya haja kubwa.
 
Aidha, amebainisha kuwa wakati wa kujifungua, mtoto huyo alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Bugando na kuwa baada ya muda mchache hali hiyo ilijirudia na kuamua kumnasua kwa kumchana bila kujua madhara ya aina yeyote ambayo yangeweza kumpata mtoto wake ambapo kwa sasa afya ya mtoto hairidhishi baada ya kuchanwa.
 
Wakazi wa eneo hilo wamesema wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa mara, huku wakithibitisha maisha ya mama huyo kuwa ni magumu kutokana na kufukuzwa na mume wake na kupata kipigo.
 
“Kwa sasa sina fedha za kununulia chakula na fedha za matibabu za kumtibu mwanangu na mimi pia kwamaana titi langu lina uvimbe, naomba wasamaria wema wanisaidie kunichangia kwa chochote walichonacho" Alisema Bi Anastazia huku akilia

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply