Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » DIWANI WA CHADEMA ATUHUMIWA KUTOA RUSHWA NDANI YA UCHAGUZI,KAHAMA.

DIWANI WA  CHADEMA ATUHUMIWA KUTOA RUSHWA NDANI YA UCHAGUZI.

*Wajumbe wachapana makonde kavu kavu,Kahama.
UCHAGUZI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,wilaya  ya Kahama mkoani Shinyanga umeingia dosari,baada ya mmoja wa madiwani wa chama hicho kuhusisha na rushwa na vitendo vya usaliti ndani ya chama kutoka CCM.
Pia katika uchaguzi huo baadhi ya wagombea wamechapana makonde huku baada ya kuenguliwa kwa baadhi ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa  Baraza la Vijana wa chama hicho (BAVICHA),huku Red Brigade wakihusika katika vurugu hizo.
Hali hiyo ilitokea jana mjini Kahama katika ukumbi wa Mamba hali, baada mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani hapa Leonard Mayala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyasubi, alienguliwa kuwania nafasi hiyo baada ya kubainika kutumia rushwa kuomba  achaguliwe katika nafasi hiyo.
Mgombea huyo alituhumiwa kutumia shuilingi milioni mbili kuwahonga baadhi ya wanachama,fedha ambazo zinadaiwa zilitolewa na baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya mtandao wa (Mpesa)ili kuhakisha  ananyakuwa nafasi hiyo.
Tuhuma hizo zimekuja  baada ya wanachama  kutokuwa na imani naye kutokana na mwenendo wa diwani huyo wa kuwa karibu na makada wa CCM wilayani hapa na hivyo kusababisha viongozi na wasimamizi wa uchaguzi huo kuengua jina lake  baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na kuwekewa pingamizi.
Aidha katika uchaguzi huo baadhi ya wagombea na wanachama walichapana makonde wakipinga kuenguliwa majina ya baadhi majina ya wagombea katika uchaguzi wa  Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA).
Ugomvi huo ulitokea baada ya wagombea waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti  wa Bavicha kuanza kujinadi kwa wananchama ndipo mgombea Thomas Masanja aliyeenguliwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kukosa sifa ikiwemo kadi yake ya uanachana kutotambulika alijitokeza na kuzuia uchaguzi.
Kufuatia kuenguliwa kwa mgombea huyo  ndipo badhi ya wafuasi wake  wakiwemo Red Brigade walipojitokeza na kuanza kufanya fujo kwa  lengo la kuzuia uchaguzi huo kuendelea wakidai kwamba mgombea wao kutotendewa haki kwa kuenguliwa kinyemela  kugombea nafasi hiyo.
Hali hiyo ilikwenda mbali zaidi  kwani wafuasi hao walianza kuwashambulia baadhi ya viongozi  na wasimamizi ambapo Mwenyekiti wa Chadema wa Halmashauri ya Msalala Emmanuel Bombeda alipingwa ngumi na Red brigade waliokuwa wakimuunga mkono  mgombea aliyeenguliwa.
Utulivu na amani urejea ukumbini humo baada ya msimamizi wa uchaguzi wa Chama hicho kanda ya Ziwa Mashairiki,Madata Sande kuingilia kati na kuwataka wanachama kuwa wavumilivu  ili kufanikisha uchaguzi huo kwani wagombea walioenguliewa katika kinyang’anyiro hicho walienguliwa kihalali  bila upendeleo wowote kwa kuzingatia katiba ya chama hicho.
Katika uchaguzi huo wajumbe walimchagua Juma Protas,kuwa Mwenyekiti wa  Chadema wa wilaya hiyo,naye Mshibu Peter akiteuliwa kushika nafasi ya Ukatibu wa chama hicho,nafasi ya Ukatibu Uenezi ikimwangukia Anord Peter na Mweka Hazina alichaguliwa,Elias Mayunga.
Nalo Baraza la Vijana BAVICHA lilimchagua Samwel Peter kuwa Mwenyekiti wake na ndani ya uchaguzi huo wajumbe walichagua viongozi mbali mbali wa yakiwemo mabaraza ya Wazee,Wanawanake na  wajumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama hicho.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply