Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » Fumanizi Babu Kubwaa!! NJEMBA YANASWA IKIVUNJA AMRI YA 6 NA MKE WA MTU, APANDA JUU YA DARI KUKWEPA KIPIGO



Mbaba Kibole Kalepe akiwa darini kuepusha kipigo baada ya fumanizi.

HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi  kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo.

Tukio hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka huu maeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole wakifanya yao.



Mke wa mtu, Asha Hemedi akihamaki baada ya fumanizi.
SIKU YA TUKIO

Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Fikiri ambaye ni dereva wa masafa marefu aliaga kwamba anasafiri lakini akiwa hajafika mbali, gari liliharibika na kurudi nyumbani kuchukua vifaa na kabla hajagonga mlango, alisikia sauti ya mkewe na Kibole.

UVUMILIVU WAMSHINDA

Chanzo hicho kilizidi kushusha mistari kwamba, baada ya kusikia sauti hizo, Fikiri hakuweza kuvumilia aliamua kuwakatisha kwa kuwagongea mlango huku akitaja jina la mkewe ili amfungulie lakini hata hivyo ilichukua muda mrefu mlango kufunguliwa.

MLANGO WAFUNGULIWA

“Mume aliendelea kugonga mlango, baada ya muda mrefu kupita ukafunguliwa ambapo mke alikutwa akiwa ameloa jasho na kuhema kwa kasi kutokana na hofu, hata hivyo alikua amefunga khanga moja tu.


MGONI JUU YA DARI

“Mume alipoangalia kila kona kumtafuta mwanaume aliyekua naye hakumuona na alipochungulia darini alimuona mgoni wake amejificha, baadaye aliomba wapigiwe simu polisi waje kumuokoa,” kilisema chanzo.

ACHIMBWA MKWARA

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, wananchi wapenda mambo ya watu waliokuwa wamezingira nyumba hiyo walimwambia yeye ni mwizi hivyo watamshushia kipondo hevi, mgoni huyo alikataa na kudai kwamba hakuwa mwizi bali mgoni hivyo wasimuue.

“Jamani mimi siyo mwizi mimi ni mgoni, niitieni polisi,” alisikika Kibole.


POLISI WAMTAITI

Wananchi walimuelewa wakaita polisi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshusha darini kisha kumkamata na mwananke wakawapeleka Kituo cha Polisi Magomeni.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply