Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » BINTI AKUTWA HAJITAMBUI KWENYE KICHOCHORO MJINI KAHAMA


Huyu ni msichana ambaye juzi alikutwa katika uchochoro wa bar ya Galax mjini Kahama mkoani Shinyanga majira ya  saa 12 asubuhi akiwa hajitambui  kutokana na kile kinachodaiwa kuleweshwa pombe na watu wasiojulikana huku nguo zake zikiwa zimechana chanwa

Baadhi ya wananchi wakimuangalia binti huyo akiwa hana fahamu  huku akiwa katika kichochoro huku nguo zake zikiwa zimechanwa na watu wasiofamika mjini Kahama. 
Askari  polisi wa kituo cha polisi Kahama Thomas Munyongo akijaribu kumtambua msichana huyo  na bila mafanikio na kuomba msaada katika kituo cha polisi .
 Baadhi ya watu wakijaribu kumtambua msichana huyo ingawa baadaye alijulikana kwa jina moja la Pili .

Baadhi ya wananchi wakimchukua binti huyo kwenda kwenye gari ya polisi na kupelekwa hospitali ya wilaya ya Kahama .

 Hivi ndivyo msichana alipochukuliwa kupelekwa hospitali ya wilaya kahama kwa uchunguzi zaidi

Baadhi ya askari polisi wamtoa msichana ndani ya gari ya polisi baada ya kumfikisha hospitali ya wilaya ya  Kahama 
 Daktari akijaribu kumkagua kama yuko hai .
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya alipinga marufuku biashara ya ngono katika wilaya yake,kutokana wasichana wengi kufanya biashara hiyo haramu .

Aidha  wilaya kahama imekuwa ni sehemu kubwa kwa wasichana kuingia katika biashara ya ukahaba jambo ambalo linafanya wasichana  wengi kubakwa na kutupwa katika mitalo ya maji au manyumba yasio kwisha

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply