Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » Stori ya kusikitisha,Mama amchinja mwanaye kisha naye auawa kwa kuchinjwa na wananchi

mauaji
Mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa kwa mapanga na wananchi wenye hasira kali kwa kitendo alichokifanya cha kumuua mtoto wake wa kambo kwa kumchinja kwa panga.
mauaji2
Mwili wa mtoto aliefariki kwa kuchinjwa na mama ake wa kambo kwa kutumia panga linaloonekana hapo chini pichani.
Tukio lilitokea hivi karibuni mkoani Mara la mama wa kambo kumchinja mtoto wake kwa kutumia panga hadi kufariki, limechukua sura mpya baada ya mama huyo nae kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kukatwa katwa na mapanga mpaka kufariki.
Tukio la kukatwa katwa mapanga mama huyo limetokea baada ya wananchi wa kijijini hapo walioshikwa na jazba kali kwa kutokubaliana na kitendo cha kinyama alichomfanyia mtoto huyo kwa kumkatishia maisha yake.
Hata hivyo wananchi walionekana kujichukulia hatua mikononi kwa kumuua mama huyo, kwa kile kilichodaiwa hawakuona hatua zozote za kisheria alizochukuliwa mtuhumuwa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.
Awali mwenyekiti wa kijiji alifuatwa na wanakijiji kuulizwa ni hatua gani ya kisheria mtuhumiwa atachukuliwa kwa mauaji ya kinyama aliyoyafanya kwamaana baada ya tukio, mtuhumiwa alionekana kutochukuliwa hatua yeyote ya kisheria kwa muda mrefu licha ya serikali ya kijiji na polisi kupata taarifa ya kutokea tukio hilo.
Mwenyekiti wa kijiji aliwajibu wanakijiji kuwa polisi wanatambua kutokea kwa tukio hilo na watakuja kumkamata mtuhumiwa na hatua za kisheria za mauaju zote zitafata juu yake.
Muda ulizidi kutokomea bila kuonekana dalili zozote za mtuhumiwa huyo kuchuliwa hatua, ndio wanakijiji wenye hasira kali walipomvamia mama huyo na kumkatakata kwa mapanga kulipiza kisasi kwa kile alichomfanyia mtoto wake.
Mwenyekiti wa kijiji analilaumu jeshi la polisi kwa kuchelewa kumchukua hatua mtuhumuwa mpaka maafa makubwa mengine kutokea.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply