Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama
ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Abdulkarim Hamis Mruma hii leo
Ikulu!.
HADIDU ZA REJEA!.
1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.
2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.
3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye
bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua
thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa
scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia
makinikia,
4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya
Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya
juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.
5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.
6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.
MATOKEO YA UCHUNGUZI
1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye
makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za
dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.
3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.
4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa
na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na
thamaninya Bilioni 13.
4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni
2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.
5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya
shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika
mrabaha
6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,
7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika
sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5
Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277
yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo
serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.
8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.
9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye
makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu
kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.
10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.
MAPENDEKEZO YA KAMATI
1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi
2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini
3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.
4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia
5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila
kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.
6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.
7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.
8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!
Hakuna maoni: