Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana
mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa
wagonjwa kwa jina la Dkt. Abdallah Juma.
Aidha, kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya
Hospitali hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma
aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na
kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama
alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa
mtego na askari wa hospitali hiyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa
Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati
mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni
madaktari kama huyo ambaye alikamatwa jana.
Hakuna maoni: