Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » 0 TAJIRI MKUBWA WA BUKOBA AFARIKI DUNIA KWENYE GARI,TAARIFA YA POLISI IKO HAPA



Inasikitisha sana kifo cha huyu bwana Leonard Mtensa kilichotokea ndani ya gari lake, mpenzi wake anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Hapa chini ni picha ya huyo dada na picha ya marehemu.

Jackline Hassan mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa na marehemu 

Huyu ndiye marehemu bwana Leonard Mtensa alikutwa na mauti ndani ya gari lake aina ya IST akiwa na mwana dada anayefahamika kama jack .

Jeshi la polisi mkoa wa Kagera linachunguza kifo cha ghafla cha Bw. Leornald Mtensa Stephen mwenye umri wa miaka  50 ambaye ni mmiliki wa club ya Lina's night club.

Tukio  hilo  limetokea mnamo tarehe 18 mwezi huu majira ya saa nne usiku maeneo ya Buyekera manispaa ya Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari ni kwamba Marehemu alikuwa katika mizunguko na gari lake lenye namba za usajili T982 CQG aina ya IST na mwana dada Jacline Hassan mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Buyekera.
Wakati marehemu akiwa na mwana dada huyo ghafla hali yake ilibadilika na kukimbizwa katika kituo cha afya cha LCT NDOLAGE iliyopo Manispaa ya Bukoba wakiwa njiani marehemu alifia njiani.
Ndani ya gari lake kulikutwa na   Wisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa marehemu.
Mwana dada Jackline Joseph anashikiliwa na jeshi la polisi hadi hapo uchunguzi utakapokamilika, sababu ya kifo hicho bado haijafahamika.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply