Serikali wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewataka wananchi wote
waliokuwa na dhamira ya kwenda kuvamia sehemu za machimbo ya madini kwa
kisingizio kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli
amewaruhusu waache kufanya hivyo mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu ameyasema hayo leo, kufuatia
taarifa ya tume ya pili ya rais ilyofuatilia athari za usafirishaji nje
wa mchanga wenye dhahabu (makinikia), iliyotolewa juni,12 mwaka huu
jijini Dar-es-salaam.
Nkurlu amesema serikali imebaini kuwepo kwa tetesi za watu wachache
kujipanga kwenda kuvamia sehemu zinazomilikiwa na wawekezaji wa migodi
hususan ACACIA na Nyang’hwale kwa madai kwamba rais Magufuli ameruhusu,
jambo ambalo siyo kweli.
Amesisitiza alichokielekeza rais Magufuli ni kwamba uzalishaji migodini
unaendelea kama kawaida chini ya usimamizi na udhibiti wa serikali na
wala siyo vinginevyo.
Tayari Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation Profesa John Thonton
amekutana na Rais Dkt John Pombe Magufuli, ambapo amekubali kuwa kampuni
yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi
ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa
kulipa kwa Tanzania.
Hakuna maoni: