Bw. Mnguni anaonekana akitafuna nywele za mwanadada huyu katika mojawapo ya mahubiri yake Afrika Kusini mwaka 2015
Kasisi
mmoja anayejiita nabii na ambaye alisababisha utata nchini Afrika
Kusini, mwaka 2015, baada ya kutuhumiwa kuwafanya watu kula nyoka, panya
na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria.
Kasi huyo alionekana katika ibada iliyoongozwa na mhubiri maarufu wa runinga nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.
Bw. Joshua ameandika katika mtandao wake wa kijamii kumhusu Mchungaji Penuel Mnguni, kuhudhuria ibada yake.
Gazeti la Afrika Kusini, Citizen, limemnukuu Bw. Mnguni akisema kuwa
amebadilisha moyo wake, baada ya kujikuta ndani ya utata na habari zake
kugonga vichwa vya habari duniani- huku akikamatwa na kuachiwa mara kwa
mara:
Hakuna maoni: