Jeshi
la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa
nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),
Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema
mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake
ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo
wilayani humo.
Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na
Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh
800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa
angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo
hakutokea.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike
Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida.
Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa
ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Singida yeye na wasaidizi wake,
fedha ambayo ilitumwa na mawasiliano yakaendelea kufanyika ili
kuakikisha kuwa siku ya tukio anakuwepo.
Cha kushangaza, siku ya tukio msanii huyo hakujitokeza na walipata
taarifa kuwa yupo Kahama anatoa huduma, walipofanya mahojiano
walithibitisha kuwa ni kweli.
Alipofanyiwa mahojiano na Polisi, Rose Muhando alikiri kutenda kosa hilo
kwa kutotoa taarifa kwamba hawezi kuja na alieleza si kweli kwamba
alikuwa Kahama, bali alikuwa na mgonjwa nyumbani hivyo hakuweza kutoka.
Muhando amesema kuwa yupo tayari kurejesha fedha hizo alizotumiwa
Hakuna maoni: