Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata amekuja nchini
kwa ajili ya kuhudhuria misa ya kumbukumbu ya watu waliofariki katika
ajali ya meli ya MV Bukoba akiwemo mama yake mzazi na binamu yake.
Matata ameamua kuacha dili la kazi aliyokuwa akitakiwa kuifanya siku ya
kesho, kazi ambayo ingemuingizia dola za kimarekani elfu hamsini.
"kweli mungu ana mitihani unaweza ukawa umekaa hauna kazi lakini pale
unapokuwa umepanga kitu, kitu kinatokea, saa ingine nasema ni mitihani
Mungu anataka kuona uko strong kiasi gani, kwahiyo kama sasa hivi,
nilikuwa nakuja huku ikatokea kazi ya hela nyingi sana, ki ubinaadamu ni
ngumu kuiachia, lakini at the end of the day lazima uwe na priority
kwenye maisha, so i had to sacrifice that for my mom na kile
kilichotokea.
Na ilikuwa ni kazi gani hasa?
Mercedes, nafanya kazi sana na Mercedes lakini ilikuwa ni kazi tofauti
kabisa wana project yao ambayo wanaifanya, kwahiyo walikuwa wameniita
kwa ajili ya hiyo kazi, wanatengeneza kitabu kikubwa kwa ajili ya
Mercedes kwahiyo walikuwa wamenichagua mmoja katika, kwasababu
kinatumika kwa muda mrefu kidogo.
For that amount of money kazi yao ulikuwa unatakiwa kuifanya kwa mda gani?
"Ni kazi unai-shoot kwa siku moja, unajua sisi tunalipwa kufatana na
mda, siku ulizoshoot kuna day rate halafu kuna usage pia na coverage
kwamba ina rushwa kwa muda gani na wapi na wapi, kwahiyo ilikuwa within
Marekani"
Tarehe 21 mwezi wa tano itaendelea kukumbukwa kwa ndugu jamaa na
marafiki waliopoteza maisha yao katika ajali ya meli ya MV Bukoba
iliyotokea mwaka 1996.
Mwanamitindo Flaviana Matata ni moja wa waathirika ambapo alipoteza mama
yake mzazi na binamu yake na amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kumbukumbu hizo zinafanyika kila mwaka.
Hakuna maoni: