Askari polisi mmoja wa kituo cha polisi Chang’ombe, Mkoa wa kipolisi
wa Temeke, ameuawa kikatili siku ya Ijumaa mchana baada ya kupigwa
risasi ya kifua na majambazi waliokuwa wanajaribu kutoroka baada ya
kufanya tukio la kihalifu. Askari hao waliokuwa doria katika eneo la
Wailes walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na majambazi hao mara baada
ya majambazi hao kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa kutumia
usafiri wa pikipiki kipindi ambapo askari polisi walikuwa karibu na eneo
la tukio. Hata hivyo wakati askari hao wakijaribu kuwafukuza majambazi
hao wawili kwa lengo la kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na
kumpiga risasi ya kifua askari huyo na kufariki pale pale.
KAHAMAYETU:Majambazi waua Askari Polisi
Hata hivyo katika harakati za kujaribu kukimbia majambazi hao
walianguka na pikipiki waliyokuwa wakitumia ndipo wakaamua kutimua mbio
mitaani na kuingia katika nyumba moja ambapo walijificha na kujifanya
kama ni wakazi wa eneo hilo, baada ya wnanchi na polisi kufika katika
nyumba hiyo, baadhi ya majirani waliwaambia polisi kwamba wameona watu
hao wameingia katika nyumba hiyo. Baada ya polisi kuingia waliwakuta
watu hao wakiwa wametulia kama kwamba wao ni wakaazi wa nyumba hiyo na
wala hawajui lililotokea.
Baada ya kuwatambua watu hao, polisi waliwatia nguvuni huku
wananchi wenye ghadhabu waking’ang’ania kuwa wanataka kuwaua sababu
wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta nikuvute kati ya wananchi na
askari hao ambao walikuwa wachache, wananchi walifanikiwa kuwachukua
majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi mwa polisi na kuanza kuwapiga
kwa silaha mbalimbali za kienyeji yakiwemo mawe na marungu mpaka
watuhumiwa hao wakapoteza maisha.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliiambia blogu hii kwamba
majambazi hayo kabla ya kupambana na polisi walikuwa wamefanya uvamizi
na kumuibia mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo. Hata hivyo mali au fedha
iliyoibiwa haikuweza kujulikana mara moja.
Hakuna maoni: