Hausigeli aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15,
ameumizwa vibaya sehemu za kichwani na kulazwa katika Hospitali ya
Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na bosi wake aitwaye
Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.
Akiongea na mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina
amesema amekuwa akipigwa na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia
waya, brenda na vifaa vingine japo alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo hivi vya ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni
siku chache baada ya hausigeli aitwaye Yusta kuripotiwa kung’atwa na
bosi wake aitwaye Amina Maige aliyepandishwa kizimbani jana katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti huyo aliyeletwa Mwananyamala jana alfajiri akiwa na hali
mbaya amefanya kazi kwa miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa
mkoani Kagera.
Melina alikuwa akiongea na mwanahabari wetu akiwa na mpira wa
kuongezewa damu mwilini na amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
matibabu zaidi.
Hakuna maoni: