Kumbe hiki ndicho kilichomfanya Wema kunyoa upara.
Wengi
walikuwa wanajiuliza kunani, haswa siku Wema Sepetu alipoamua kunyoa
Dongo, huku kila mtu akitoka na story yake mwenyewe kwa mtazamo tofauti
bila hata kujua sababu halisi ya uamuzi wake huo, ila ukweli ni kwamba,
Diva
huyu ni moja kati ya wasanii wanaochukua kazi yake very serious, na hii
ndio siku alipoamua kupotezea urembo wake na kuvaa uhusika wake
uliomlazimisha kuchukua hatua hiyo ya kunyoa Upara,
Akiwa
anaongea katika nyakati tofauti alisikika akifunguka kuwa, Movie mpya
yake anayoifanya iitwayo Family ndio iliyomfanya anyoe upara, huku
akielezea kuwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na uhusika aliotakiwa
kuvaa, uliokuwa unaelezea mtu mwenye Saratani.
Wema
ni moja kati ya wasanii wachache ambao hadi hii leo wana uwezo wa
kufanya hivi ili tu kufikisha maudhui ya story iliyokusudiwa kwa jamii
Hakuna maoni: