Mkazi mmoja wa Kijiji cha Lundusi
Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi Scholastica Mhagama
amesema miaka mingi ameishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa bila msaada
kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe
ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia.
“Kila siku naomba Mwenyezi
Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata,
lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo
maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
“Nimetengeneza kabisa jeneza
langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka ili
kuepukana na mateso haya. Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa
kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne
walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa masikitiko.
Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja.
“Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” anasema
Hakuna maoni: