mashindano ya mbio za baiskeli yafana kahama
Mgeni rasmi naibu waziri wa utamaduni na
michezo Juma Nkamia Akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa kahama kwenye
mashindano ya mbio za baiskeli ambayo yamefadhiliwa na Mgodi wa African
barrick Gold mine Buzwagi
Mbuge wa kahama jemes lembeli akitoa
salamu kwa wakimbiza baiskeli kabla hajamkaribisha mgeni rasim Naibu
waziri utamaduni na michezo Juma Nkamia .
Baadhi ya umati mkubwa uliojitokeza kuona mashindano ya mbio za baiskeli katika uwanja wa taifa kahama .
Mshindi wa pili toka shinyanga akibidhiwa kikombe na mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya
Mshindi wa tatu toka mwanza mbio za
Baiskel akipokea fedha tasilmu laki saba toka kwa meneja wa mgodi wa
Buzwagi Filber Rweyemamu .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya
akimpokeza mshindi wa tatu toka musoma na nyuma yake ni meneja wa mgodi
wa Buzwagi Filber Rweyemamu mwenye kofia nyuma ya mkuu wa wilaya ya
kahama
Mshindi wa kwanza kwa mwanawake Matha
Anthony ambaye alikibia kilometa 80 toka kahama hadi kijiji cha
sungamile ambapo alipata fedha taslmu milioni moja .
Mshindi wa pili Seni konda toka
shinyanga alinye na bahasha akibidhiwa na Naibu waziri wa utamaduni na
michezo Juma Nkami wa kati ana alishika medal ni makamu wa Rais wa
African Barrick Gold mine.
Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli
masunga Duba ambaye alikimbia kilometa 156.5 toka kahama hadi tinde
kwenda na kurudi ambapo alijinyakulia fedha taslmu milioni moja na nusu
mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya
akimbidhi mshindi wa mbio za baiskeli kwa mwanawake za kilometa 80 matha
Athony kujinyakulia milioni moja.
picha ya pamoja naibu waziri wa
utamaduni na michezo juma Nkamia mwenye kofia mbele ya mshindi wa pili
mwenye bahasha mkononi seni konda ambaye alinyakulia kitita cha milioni
moja .
mshindi wa pili wa mbio za Baiskeli Seni
konda akinua mikono juu baada ya kukabidhiwa kikombe na fedha milioni
anaye piga makofi ni makamu wa Rais wa( ABG)Deo mnyika katika viwanja
vya halmashauri ya kahama (Marufu uwanja wa Taifa )
Mashindano ya mbio za
baskel wilayani kahama mkoani shinyanga yazidi kutimuwa vumbi katika viunga
mbalimbali wilyani humo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji wa Madini
African Barick Gold.Kupitia mgodi wa dhahabu Buzwagi ABG wakishirikiana na
chama cha waendesha Baiskel Tanzania.
Mashindano hayo
yaliyokuwa pata shika nguo kuchanika kutafuta mshingi wa kwanza hadi wa
ishirini kwa wavulana pamoja na wasichana ambapo yalikutanisha mikoa 6 ya kanda
ya ziwa ambayo ni Mara, Mwanza ,
Geita,Kagera, Simiyu pamoja na shinyanga.
Katika mbio hizo za
baiskeli zilizowakutanisha washiriki wa jinsia zote huku wavulana wakikimbia
kilometa 156.5 kutoka maeneo ya faphtom kuelekea manzeshe hadi shinyanga
vijijini ambapo wasichana wakikimbia kilometa 80 kutoka maeneo ya faphtom
kuelekea manzese hadi Sungamile Isaka,huku wote kumalizia mashindano hayo
katika barabara ya Bijampola mjini
kahama.
Kwa upande wake katibu
Mkuu Taifa chama cha waendasha baiskeli
John Machemba awali akizungumza katika ufunguzi wa mbio hizo wilayani humo
amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutafuta washindi 20 kutoka pande zote
mbili kwa wanaume pamoja na wanawake ili kwenda kushiriki katika shindano
lililoandaliwa huko mbeya litakalo shirikisha kanda 6.
Machemba alimtanganza
mshindi wa kwanza kuwa Masunga Duba kutoka mwanza aliyekimbia
masaa 4 na sekunde 3 huku akipata zawadi ya shillingi million 1.5, Medali
pamoja na kikombe huku mshindi wa pili akitajwa kuwa ni Seni Konda kutoka
shinyanga huku akipatia Tsh.million 1 na Medali pamoja na Kikombe.Pamoja na
mshindi wa 3 Simon Mbaluku kutoka simiyu akipatiwa Tsh,laki 7.
Huku Mshindi wa 4
hadi wa 10 walipatiwa Tsh.laki 2.5 pamoja na wengine waliobaki ambao
hawakuingia katika kumi bola walipatiwa Tsh,laki 1.5 ili kuwahamasisha
kushiriki katika mashindano mengine kwa mwaka ujao.
Kwaupande wake Makamu
wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini African Barick Gold.Kupitia mgodi wa
dhahabu Buzwagi ABG,,Deo Mwanyika amesema kuwa kampuni hiyo inawajali wananchi
huku lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji mbalimbali ya vijana huku akiwataka
kutumia fursa hiyo ili kutambua uwepo wawawekezaji katika maeneo yao
Nae naibu waziri wa
habari,utamaduni vijana na michezo Juma Nkamia ameitaka halmashauri ya mji wa kahama kutumia fursa
hiyo ya wawekezaji kukuza vipaji mbalimbali ya vijana ikiwa ni pamoja na
kubolesha mazingira ya michezo hususani uwanja
wa michezo wa halmashauri hiyo.
Pia ameutaka uongozi
wa mgodi huo kushirikiana na ofisi yake katika kuulekebisha uwanja wa michezo
wa halmashauri hiyo huku mgodi ukibolesha uzio(UKUTA) na ofisi yake
ikipandikiza majani ya bandia pamoja na kubolesha mazingira ndani ya uwanja
huo.
Hakuna maoni: