Wazazi
wengi Afrika wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi
wanapokua kwenye hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni
kwamba ukiongea na watu ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo
kama mpira wa miguu, ama kuimba na vinginevyo utagundua kwamba jitihada
binafsi zimewaongoza kugundua vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo
ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye
ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto
waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft
unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni
mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya
Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika
mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy
kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na
kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa
na Microsoft ambaye ana umri mdogo zaidi duniani.
Hakuna maoni: