Sina
Baba wala Mama, naishi na bibi yangu mzaa mama simjui baba yangu, mama
yangu alifariki, sisomi shule, sina madaftari wala nguo za
shule,nachunga ng’ombe wa jirani yetu, bibi yangu ni mkulima, tunapata
chakula kwa kubangaiza, siku nyingine tunalala na njaa, bibi yangu ni
mzee sana.
Ni kauli ya mtoto huyu(aliyejitambulisha kwangu jina lake)anayefikia umri wa miaka 12 mkazi wa kijiji cha wavuvi na wafugaji (katika eneo hili nililotembelea)ambaye kwa kawaida alipaswa kuwa shuleni akipata elimu.
Familia
nyingi za maeneo ya vijijini zimekuwa katika kadhia za aina hii, maisha
ya sulubu ndiyo waliyoyazoea, wameyakubali na kuyafanya kuwa ni sehemu
ya maisha yao ya kila siku.
Ni
nadra kwa mtu wa kawaida kuyazoea maisha ya aina hii lakini ipo jamii
ambayo imelazimika kuyakubali na kuyapokea maisha haya na kuyafanya kuwa
ni sehemu ya maisha yao ya kawaida.
Ni
vigumu kuizoea hali hii lakini haya ndiyo maisha ambayo jamii hii
imeyazoea na kuyakubali aghalabu familia nyingi za mjini huishi maisha
yenye nafuu ingawa pia huikumbana na dharuba za kila siku za kuishi
chini ya dola moja, ni tabaka la watu wa kawaida, nao wameyazoea na
kuyakubali maisha ya aina hii.
Unaweza
kuyakubali au kuyakataa maisha ya iana haya lakini mazingira halisi ya
kipato yanakushawishi uyakubali na uishi katika hali hiyo kwa kadri
ambavyo Mungu amekujaalia.
Kilio
cha jamii hii kinapaswa kuelekezwa wapi? Katika jamii yenyewe au kwa
washika dhamana kwenye mhimili mkuu, walioshika mpini wakawapa makali
walalahoi ili wagombanie kukatwa mikono yao.
Hakuna maoni: