Muonekano wa
Chuo hicho.
Mwanafunzi
mmoja wa kike kutoka Chuo cha Moi huko Eldoret, Kenya amekutwa amefariki dunia
karibu na moja ya hosteli za chuo hicho baada ya kubakwa na kuuwawa kikatili.
Mwanafunzi
huyo inasemekana kuwa ni wa mwaka wa tatu chuoni hapo akichukulia masomo ya Sanaa
na Sayansi ya Jamii.
Tukio hilo
la kinyama, limetokea usiku wa kuamkia Jana Februari 22,2015 na bado polisi haijawatia hatiani
washtakiwa ama wahusika wa tukio hilo. Habari za mkasa huo zinazidi kuenea kila
kona ya chuo, huku taharuki na hofu kubwa ikizidi kuwapanda wanafunzi wengine
wa kike ambao wameamua kupaza sauti kuuomba uongozi wa chuo hicho kuimarisha
suala zima la ulinzi kwa usalama zaidi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wanafunzi wa zamani katika chuo hicho, wamethibitisha kuwa
tangu mwaka 2006, kumekuwa na matukio ya aina hiyo ambapo wanafunzi wengi
wamekuwa wakikabwa na wengine kubakwa na watu wasiofahamika mara moja, hivyo
wanafunzi kuwabatiza jina la ‘mashoka’,kutokana na wakabaji kutumia silaha za
shoka katika kutekeleza azma yao.
Hakuna maoni: