Mkuu
wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewaongoza mamia
ya wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji kuaga miili ya watu wanane
wakiwemo wanafunzi sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya
Kibirizi Mjini Kigoma wali fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi
kufuatia mvua iliyonyesha kwa takribani masaa matatu.
Majonzi
yalitawala shughuli hiyo hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika
viwanja vya shule ya msingi Kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari
kwa maziko huku mwili wa Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda Moshi kwa maziko .
Akitoa
salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa
Machibya amewataka wafiwa na wananchi kuchukulia tatizo hilo kama ni
tukio la ajali ya kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.
Kwa
upande wao viongozi wa dini Sheikh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na
mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba
huo,
wamewataka waumini wa dini mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila
mwanadamu ataonja mauti kwa wakati wake na kwamba imani za kishirikina
zisihusishwe katika msiba huo.
Hakuna maoni: