Adhabu
ni sehemu ya maisha katika malezi ya watoto lakini imekuwa tofauti kwa
wazazi hawa kutoka Japan ambao waliamua kumuadhibu mtoto wao mwenye umri
wa miaka (7) Yamato Tanooka, kwa kumuacha katika msitu wa kisiwa cha
Hokaido ambapo ni makazi ya wanyama pori baada ya kumkuta na kosa la
kurushia mawe magari yaliyokuwa jirani yao.
Kikosi
cha waokoaji zaidi ya 150 bado kinaendelea na msako huko Nanae Japan
ikiwa leo ni siku ya tatu tangu apotee. Wazazi wa mtoto huyo wamekiri
kufanya hivyo ila haikuwa dhumuni lao kumuacha kwa muda mrefu kwani
walirudi eneo la tukio muda mfupi tangu wamuache ila walipofika
hawakumkuta.
Mwanzoni
baba wa mtoto huyo aliripoti kupotea kwa mwanae walipokuwa wanatafuta
mboga, lakini baadae akaamua kuwaambia polisi ukweli na kusema
walimshusha kwenye gari kama kumpa adhabu tu. Mpaka sasa polisi
wanafikiria juu ya swala hili na huenda wakafunguliwa kesi ya
‘Utelekezaji wa mtoto‘
Home
»
»Unlabelled
» Makubwa Haya!! Mtoto Wa Miaka 7 Atupwa Msituni na Wazazi Wake Kisa Kapiga Mawe Gari la Jirani
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: