Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ameonya
wakandarasi wanaojenga miradi ya maendeleo chini ya kiwango jimboni
kwake, na kutaka miradi hiyo waijenge kwa hadhi ya juu kulingana na pesa
wanazopewa na siyo kuilipua na kuingizia hasara serikali fedha za
matengenezo ya mara kwa mara.
Masele
ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua miradi ya Maendeleo
inayotekelezwa jimboni mwake na kukuta mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba
ya walimu katika shule ya sekondari Masekelo ambayo itakuwa na uwezo wa
kuhifadhi walimu Sita, kutaka kujengwa chini ya kiwango kutokana na
Matofari na kokoto kutokuwa na ubora.
Mheshimiwa
Masele amekagaua miradi ya ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa Mawili,
Matundu ya vyoo 18 katika shule hiyo ya Masekelo, na ukaguzi wa ujenzi
wa barabara ya Tanroad km 2.3 na zile zinazojengwa katikati ya mji
Kilomita 13.1 na kuwataka wakandarasi wote kujenga miradi hiyo kwa
kiwango kinachotakiwa.
“Mkurugenzi
mkandarasi huyu anayetaka kujenga nyumba hii ya walimu chini ya
kiwango, kwanza tofari na hizi kokoto aziondoe aweke tofari zingine tena
na ujenzi wake asimamiwe kikamilifu maana asije akalipua kazi na hapo
baadaye nyumba hii ikaja kuleta maafa”, amesema Mheshimiwa Masele.
“Pia
naagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Maendeleo kwenye jimbo
langu waijenge kwa kiwango kinachotakiwa na siyo kulipua kazi ili
miradi hii ipate kudumu kwa muda mrefu na kutekeleza miradi mingine
ambayo itaondoa kero kwa wananchi na kuufanya mji wa Shinyanga kuwa wa
kisasa na kukua kiuchumi”,ameongeza Mheshimiwa Masele
Naye
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna
amesema mkandarasi anayejenga nyumba hiyo ya walimu alishamwambia aondoe
tofari hizo na kokoto lakini amekuwa mkaidi, huku akibainisha kwa
mkandarasi atakaye jenga miradi chini ya kiwango atakuwa amejiondoa
kupata kazi tena .
Angalia picha hapa chini ziara ya mheshimiwa Masele leo jimboni kwake
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akiwa na
mkurungezi wa halmshauri ya manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna
wakikagua matundu vya vyoo 18 vilivyomalizika kunjengwa katika shule ya
sekondari Masekelo iliyopo katika manispaa hiyo.Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Zoezi la kukagua matundu ya vyoo likiendelea
Mheshimiwa Masele akikagua choo
Mheshimiwa Masele (kulia) akiteta jambo na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna
Mheshimiwa Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa sekondari Masekelo
Mheshimiwa Masele na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakielekea kwenye eneo panapojengwa nyumba ya walimu
Mheshimiwa
Masele akikagua ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo itahifadhi walimu
sita itakayokamilika mwezi Julai mwaka huu na kughalimu shilingi
milioni 150 ambapo ndipo amebaini matofari na kukoto zinazotumika
kujenga nyumba hiyo hayana ubora na kuagiza tofari na kukoto ziondolewe
ziletwe zenye kiwango bora.
Mheshimiwa Masele akiwa eneo la ujenzi na mhandisi wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo
Masele
kushoto katikati Mkurugenzi mwisho mhandisi Simon Ngagani (kulia)
wakiangalia darasa lililomalizaka kujengwa kwenye shule hiyo ya Masekelo
Mheshimiwa Masele akiwa nje ya darasa hilo
Mheshimiwa
Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome
kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na
kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.
Mheshimiwa
Masele akizungumza na wanafunzi wa shule ya Masekelo na kuwataka wasome
kwa bidii il iserikali hapo baadae ipate wataalamu wake pamoja na
kufanikiwa katika maisha yao na kusaidia wazazi wao.
Mheshimiwa Masele akiwa katika eneo la miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami km 2.3
Mheshimiwa
Masele akikagua miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami km
2.3 huku akitoa Maelekezo ujenzi huo ujengwe kwa kiwango kinacho takiwa
ilibarabara hizo zidumu kwa muda mrefu, Kulia kwake ni Paulo Saitabu
mshauri wa ujenzi wa barabara hiyo ya Tanroad akipokea Maelekezo hayo ya
ujenzi kwa kiwango cha juu.Kushoto ni Godfley Set ambaye ni Msimamizi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya JASCO
Mheshimiwa Masele akitoa maelekezo
Mheshimiwa Masele akikagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami
zinazojengwa katika kati ya mji wa Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya
Dunia zenye urefu kilomita 4.4 na kutarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka
huu chini ya Mkandarasi (JASCO) ambaye pia atajenga barabara ya Km 13
katika manispaa hiyo kwa thamani ya shilingi bilioni 15.4
Mbunge
Masele akiwa na diwani wa viti maalumu tarafa ya Ibadakuli Zuhura
Waziri wakibadilisha mawazo wakati wakikagua Jenzi hizo za barabara kwa
kiwango cha lami katikati ya Mji wa Shinyanga.
Masele akiendelea kukagua ujenzi wa barabara
Mheshimiwa Masele akiendelea na zoezi la ukaguzi
Mbunge Masele akisalimiana na wapiga kura wake na kuwaahidi mambo mazuri ikiwa ndiyo amekuja kuanza kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake
Wapiga kura wakifurahia jambo
Mbunge Masele akisalimia na wapiga kura wake
Mheshimiwa Masele akiongea na wananchi
Mbunge Masele akisalimiana na mwananchi
Hakuna maoni: