JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo
wanawake wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya
sekondari Mwika wilayani Moshi, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia
silaha.
Miongoni mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10,
waganga wa kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa
dawa watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na kuzindika silaha
zilizokuwa zikitumika katika ujambazi na wanawake wapishi wa watuhumiwa
hao wakiwa mafichoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mtafungwa alisema jana
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya
Tanga na Kilimanjaro kufuatia msako mkali wa askari uliotokana na
taarifa za siri.
Mtafungwa alisema mwanafunzi wa sekondari ya Mwika, Kelvin Shayo (17)
miongoni mwa matukio anayotuhumiwa kushiriki ni pamoja na la kumpora
bastola yenye namba YP0466 Tz Car aina ya brown, askari mstaafu wa Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Elibariki Urio (67).
Kamanda alisema silaha hiyo iliporwa Februari 25 mwaka huu baada ya
majambazi kumvamia nyumbani kwake na kupora mali pamoja na silaha hiyo
kisha kwenda kuificha nyumbani kwa Eleutery Nguma (62) mkazi wa Makami
Chini, Tarafa ya Vunjo ikiwa imefukiwa ardhini kwenye mfuko wa plastiki.
Aidha, Mtafungwa alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za polisi mtuhumiwa
huyo (Nguma) ilidhaniwa kuwa ameacha vitendo vya ujambazi lakini
amebainika kuwa ni mpangaji wa njama za ujambazi, kuficha mali za wizi
pamoja na kuficha silaha zinazotumika katika uhalifu.
Home
»
»Unlabelled
» Watu 14 Wakamatwa Kwa Tuhuma ya Ujambazi Huko Kilimanjaro,Yumo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwika
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: