Hayo yamesemwa jana na katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga wakati akitoa tamko la UWT wilaya hiyo kwa rais Magufuli na makamu wa rais Samia Suluhu kwa kuchaguliwa na kwa utekelezaji mzuri wa kazi zao tangu kuchaguliwa kwao katika uchaguzi mkuu uliopita.
Haule alisema umoja huo unampongeza rais Magufuli na makamu wa rais kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuijengea heshima nchi tangu walipochagulia hali iliyosababisha nchi na Chama Cha Mapinduzi kujipatia heshima kubwa.
“Rais Magufuli ameijengea heshima kubwa nchi yetu kwa kuimarisha na kujenga upya misingi ya uongozi na uwajibikaji iliyoanzishwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage,hali hii imewafanya wananchi kuwa na imani na serikali yao kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika Nyanja zote”,alieleza Haule.
Aidha Katibu huyo wa UWT,alisema kuwa wanatoa pongezi kwa hotuba nzuri ya kwanza ya rais Magufuli aliyoitoa yenye kuonesha malengo,kuthubutu,jitihada na mwelekeo na dira ya serikali ya awamu ya tano aliyoitoa wakati wa akihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20.11.2015.
Haule alisema UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini imeridhishwa na utaratibu wa rais Magufuli katika nidhamu ya matumizi ya fedha pia kupambana na mafisadi wakiwemo wala rushwa kazi ambayo ni kubwa na ngumu lakini kwa hatua aliyofikia inatia matumaini makuwa kwa wana CCM na Watanzania kwa ujumla.
“Kutokana na utendaji wa mheshimiwa rais akishirikiana na makamu wa rais na watendaji mbalimbali wa serikali nchi mbalimbali zimejenga imani kubwa kwa nchi yetu”,aliongeza Haule.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika kikao hicho,kaimu katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Solomon Itunde aliwataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanakuwa makini katika uchaguzi wa viongozi wa CCM mwaka 2017 ili kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu 2020.
“Tukichagua viongozi sahihi katika uchaguzi wa ndani ya CCM mwaka ujao,itatusaidia kushinda uchaguzi mkuu 2020 kwa urahisi zaidi kwani viongozi hao watapigania maslahi ya chama kwa nguvu zao zote”,alieleza Itunde.
Hata hivyo Itunde aliwapongeza wanawake wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa kusimama kidete katika uchaguzi mkuu uliopita hali iliyosababisha kata zote 26 za wilaya hiyo kuchukuliwa na CCM huku kiti cha Ubunge jimbo la Solwa nacho kikichukuliwa na mgombea wa CCM Ahmed Salum.
Mbali na kujadili mambo kadha wa kadha ya kujenga Chama,
UWT wilaya ya Shinyanga vijijini wamechangia utoaji wa damu kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuondoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi sababu ya kukosa wa damu.
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga inakabiliwa na tatizo la uhaba wa damu kwani kila siku hutumia uniti 20, kwa wiki uniti 150 hali ambayo ni hatari hususani kwa akina mama wajawazito na watoto ambao ndiyo wahitaji wakubwa wa damu hiyo.
Kaimu mratibu wa damu mkoa wa Shinyanga Felix Manda aliupongeza umoja huo wa wanawake wa (CCM) Kwa moyo waliouonyesha wa kuchangia damu, ikiwa hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo hilo kwa asilimia kubwa ambapo inatakiwa kwa wastani kuwe na Uniti 150 kwa wiki.
Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo katika kikao hicho,ametuletea Picha 22 wakati wa kutoa tamko hilo na akina mama wa UWT wakichangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto..Tazama hapa chini
Aliyesimama ni mjumbe wa UWT taifa Dr. Christina Mzava akizungumza katika kikao hicho
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akichangia damu
Hakuna maoni: