MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 14 kwa wakuu wa
wilaya kuhakikisha wanawapatia sehemu ya kufanyia biashara wamachinga
wote wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara.
Pia amewataka wale ambao tayari wamepatiwa maeneo kurejea katika maeneo yao na kuondoa biashara zao pembezoni mwa barabara.
Makonda
alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini
hapa ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kutoitumia vibaya kauli ya
Rais John Magufuli kwa kuwa tayari wameshatengewa maeneo lakini waliamua
kurejea baada ya kauli hiyo.
“Rais
wetu alisema wasibughudhiwe ila watengewe maeneo maalumu kwa ajili ya
kufanyia biashara zao, maeneo tumeshatenga hivyo ni vyema wakarejea
katika maeneo yao na wale ambao hawana kabisa waonane na wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi ili wapatiwe maeneo,” alisema.
Alisema
uwepo wa wafanyabiashara hao katika maeneo ya hifadhi ya barabara
kumesababisha kero na misongamano isiyo ya lazima inayowanyima uhuru
watembea kwa miguu.
“Hatukuweka
lami ili utandike bidhaa zako barabarani, watembea kwa miguu wanateseka
kwa sababu yenu vibaka wameongezeka watu wanaibiwa kila kukicha nitoe
wito tu muondoke wenyewe na hatutapenda kutumia nguvu kuwaondoa,”
alisema Makonda.
Aliongeza
kuwa kuwepo kwa wamachinga hao kumeisababishia Manispaa ya Ilala
kupoteza mapato kwa kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao sio
waaminifu wakiwatumia wafanyabiashara hao kuuza bidhaa zao na kukwepa
kulipa kodi.
“Wamachinga
wamekuwa wakitumika kupitisha mizigo kwa njia zisizo sahihi, kuna watu
wanawakusanya na kuwapeleka kwa wafanyabiashara wakubwa na kuwapatia
bidhaa jambo linalosababisha bidhaa hizo kuuzwa bila kulipiwa kodi,”
aliongeza Makonda.
Aidha
Makonda alisema jiji hilo lina mpango wa kuweka maeneo maalumu
yanayoonesha bidhaa za ndani na zile zinazotoka nje ya nchi.
Home
»
»Unlabelled
» MAKONDA AWAGEUKA MACHINGA DAR,AWAPA SIKU 14 KUONDOKA BARABARANI
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: