Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi
Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na
mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni
ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe
msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio
anaetegemewa, yaani ndio star kwao.
Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa
ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka
kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe
kwa jinsi anavyowaendekeza.
Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na
wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na
ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu
masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka
najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na
mahindi) nalima mwenyewe.
Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake
na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya
kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha
yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati
kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya
chakula kabisa.
Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda
niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha
familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na
ninaomba ushauri wenu ndugu ; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home
na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa
marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili,
anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki,
anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje
tuishi nae hapa home.
Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea
maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa,
ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto
wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato
wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka
sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.
Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi
uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata
ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta
mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.
Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha
ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu,
natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena
roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume
huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine
ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na
hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni
maisha ya mjini (u can imagine)!
Msaada jamani!
Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress
By Sisame
Topics: burudani
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: