MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta akiishiwa pozi baada ya kupata taarifa kuwa, msichana ambaye aliwahi kujianika kufanya mambo ya usagaji, Malkia Said ‘Malkiz’ amemzimikia na yupo tayari kuolewa naye hata mke wa nne.
Ishu hiyo ambayo ilizua viulizo ilijiri siku chache zilizopita ambapo mwanadada huyo aliweka ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, akishikilia msimamo wake wa kuacha usagaji na kudai kwa mara ya kwanza amejikuta akipagawishwa na Nuh japo ni mume wa mtu.
Malkis alipoulizwa alisema; Pale nilivyoandika nilisema nilikuwa nimelewa, lakini nikuhakikishie sikukosea kuandika vile nikiwa kama binadamu mwenye hisia, niliona niweke wazi hisia zangu, sijawahi kuvutiwa na mwanaume ila Nuhu natamani hata anioe sababu dini yetu ya Kiislamu inaruhusu wake wanne na nipo tayari kubadilika hata kimavazi.”
Nuh alipotafutwa kuhusiana na jambo hilo alistaajabu na kujikuta akiangua kicheko mwanzo mwisho, kisha akaomba shushushu wetu amuache kwanza kwa kuwa hakuwa na cha kujibu
Hakuna maoni: