Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi
Mauaji ya walinzi mkoani Geita yameendelea kuwa tishio kwa usalama wao
baada ya mlinzi mwingine aliyekuwa akilinda maduka yapatayo 15, kuuawa
kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Mauaji
ya mlinzi huyo Kisusi Iddy (40) aliyekuwa akilinda maduka hayo kwenye
Mtaa wa Mwatulole, ni muendelezo wa matukio ya kuuawa walinzi wa maduka
na mali mbalimbali kwani katika kipindi cha miaka miwili jumla ya
walinzi 20 wameuawa.
Taarifa
zilizopatikana jana kuhusu mauaji ya mlinzi huyo na kuthibitishwa na
mwenyekiti wa mtaa huo, Fikiri Toi zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia Januari Mosi na wauaji hao hawakuiba kitu chochote.
Mwili wa Iddy ulikutwa umefunikwa kwa shuka lake alilokuwa akilitumia lindoni, huku likiwa limetapakaa damu.
Kutokana
na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amefuta vibali vyote vya
waganga wa tiba za asili kwa madai wao ni moja ya chanzo cha imani za
kishirikina zinazosababisha mauaji hayo.
Alisema
kutokana na kukithiri kwa mauaji hayo, mamlaka yake inakusudia kufufua
Jeshi la Jadi (Sungusungu) ili kusaidia kuyadhibiti.
Hata
hivyo, Kapufi alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa wakati wa uhai
wake, Iddy alikuwa analinda maduka ya wafanyabiashara yanayofikia 15 na
kwamba baada ya kufuatilia, hakuwa na mafunzo yoyote ya ulinzi.
Aliyepigwa na wafugaji Moro afariki
Fabian
Bago (21) anayedaiwa kushambuliwa na wafugaji katika Kijiji cha Kolelo,
Morogoro, amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro
alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Frank Jacob alisema kijana huyo alifariki
dunia saa 11 jioni jana akiwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji
uangalizi wa karibu na kwamba mwili wake umehifadhiwa kusubiri taratibu
nyingine za kipolisi.
Dk
Jacob alisema mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, kijana huyo
alifanyiwa vipimo na matibabu lakini alifariki dunia kutokana na
majeraha makubwa kichwani yaliyoharibu sehemu ya ubongo.
Baba
mzazi wa kijana huyo, Alan Bago alisema ameshatoa taarifa polisi
kuhusina na kifo cha kijana wake na sasa anasubiri maelekezo ya polisi
ili aweze kuendelea na taratibu za mazishi.
Hakuna maoni: