Muimbaji wa Brazil, Loalwa Braz, aliyejipatia umaarufu kwa wimbo wake wa mwaka 1989 ‘Lambada’, amekutwa amefariki kwenye gari iliyoungua moto mjini Rio de Janeiro.
Loalwa Braz akiwa na Akon backstage mwaka 2012 kwenye tuzo za Billboard Latin Music Awards, Miami, Florida
Mwili wa muimbaji huyo aliyekuwa na miaka 63 ulikutwa karibu na nyumbani kwake huko – Saquarema.
Polisi bado hawajaweza kutambua sababu ya kifo chake.
Polisi bado hawajaweza kutambua sababu ya kifo chake.
Braz alikuwa muimbaji mkuu wa kundi Kaoma lililokuwa na makazi Ufaransa na Brazil na , lililopata umaarufu kwa wimbo Lambada. Msanii wa Marekani, Jennifer Lopez aliwahi kusample wimbo huo kwenye hit yake ya mwaka 2010, On The Floor
Hakuna maoni: