Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Januari 13,2017 amefungua rasmi
viwanda viwili mkoani Shinyanga.
Rais Magufuli amefungua Kiwanda cha
kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya
Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited na kiwanda cha Jambo
Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji
baridi ikiwemo soda,juisi na maji.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde ametusogezea picha 45 wakati wa uzinduzi wa viwanda hivyo
Katikati ni rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha
kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya
Sandarusi cha Fresho Investment Company limited kilichopo katika
manispaa ya Shinyanga,kulia ni mkurugenziwa kiwanda hicho Freddy Shoo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza
vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho
Investment Company Limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wananchi wa
mkoa wa Shinyanga waliofika katika kiwanda Fresho Investment Company
Limited kushuhudia uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kiwanda hicho.Kulia kwake ni mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kushikana mkono na mkurugenzi
wa kiwanda cha Fresho Investment Company limited Freddy Shoo baada ya
kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa kiwanda hicho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kukata utepe kuashiria kufungua
rasmi kiwanda cha kutengeneza mifuko ya sandarusi cha Fresho Investment
Company Limited.
Rais Magufuli akikata utepe kuashiria
kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho
Investment Company Limited cha Mkoani Shinyanga.Kushoto wa kwanza
kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele,wa tatu ni
mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wa kwanza kulia ni mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Kishapu
Suleiman Nchambi,mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kiwanda cha Fresho Investment
Company Limited akiongozwa na mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho
Investment Company Limited Freddy Shoo (kushoto) akimwonesha rais
Magufuli jinsi uzalishaji wa vifungashio/mifuko ya sandarusi
unavyofanyika katika kiwanda hicho
Rais Magufuli akiangalia mifuko ya sandarusi katika kiwanda hicho
Rais Magufuli akiangalia mifuko/vifungashio vya bidhaa mbalimbali vilivyotengenezwa katika kiwanda hicho
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho
Investment Company Limited Freddy Shoo akimwelezea rais Magufuli namna
mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho inavyofanya kazi katika
kiwanda hicho
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho
Investment Company Limited Freddy Shoo akiteta jambo na rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha
Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko
ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited ambapo alisema
kiwanda hicho ni kizuri na cha kisasa huku akimpongeza mmiliki wa
kiwanda hicho Freddy Shoo ambaye ni Mtanzania kwa kuunga mkono jitihada
za serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza rais
Magufuli ambaye alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania wengine wenye
pesa kujitokeza kuwekeza katika viwanda ili kuhakikisha kuwa uchumi wa
nchi unakua na wananchi wanapata ajira
Tunamsikiliza rais Magufuli
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (mwenye ushungi mweupe katikati)
wakimsikiliza rais Magufuli
Hapa
ni ndani ya kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi ikiwemo soda,maji
na juisi cha Jambo Food Products Company Limited.Katikati ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho ambacho awamu ya kwanza
ya ujenzi wake ulianza mwaka 2015 na kukamilika Juni 2016 kwa kuanza na
uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,Malta,Fresh Juice,Energy
drinks na maji kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 kwa siku
Kushoto ni mkurugenzi wa kiwanda cha
Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi
akimweleza rais Magufuli namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi.Pamoja na
mambo mengine alisema awamu ya pili ya ujenzi itakamilika Oktoba 2017
ambapo kiwanda hicho kitaweza kusindika na kufungasha matunda yote
yaliyopo kanda ya ziwa Victoria
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food
Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi ambaye ni
mbunge wa Meatu mkoani Simiyu akimwelezea rais Magufuli jinsi mfumo wa
komputa unavyofanya kazi katika shughuli za uzalishaji katika kiwanda
hicho cha vinywaji baridi
Rais Magufuli akiwa katika kiwanda cha
Jambo Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga ambacho
asilimia 100 ya umiliki wake ni watanzania wazawa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
soda zilizozalishwa katika kiwanda hicho zikiwa tayari kwa ajili ya
matumizi
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food
Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akitoa hotuba
fupi kuhusu kiwanda hicho.Alisema uwekezaji utakapokamilika mwezi Oktoba
mwaka huu,utakuwa na thamani ya dola 125,000,000.Mbuzi aliwataja
waliofanikisha katika ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni Benki ya CRDB
(Tanzania),COMMERZ Bank (Germany),Krones (Germany),Volvo(Tanzania) na
EKN Bank ( Sweden)
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food
Products Company Limited Salum Mbuzi alimshukuru rais Magufuli kufungua
kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kuunga mkono kwa vitendo jitihada za
serikali ya awamu ya tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda
Wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi wa
kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi ambapo
alisema tayari kiwanda hicho kimetoa ajira rasmi 365 na zisizo rasmi 500
na matarajio ni kufikia ajira 2500 pindi uwekezaji utakapokamilika na
kwamba hivi sasa bidhaa zao wanauza ndani ya nchi na wanatarajia kupanua
masoko ya nje ya nchi kwa nchi za Burundi,Rwanda na Kongo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food
Products Company Limited ambapo aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho
kumuunga mkono kwa vitendo kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya
viwanda badala ya kuendelea kutegemea viwanda vya nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli alieleza furaha yake kuona mkoa wa Shinyanga
ukiwa kituo cha uzalishaji wa vinywaji huku akiwapongeza viongozi wa
mkoa wa Shinyanga kwa kumuunga mkono kwa vitendo na kuahidi kuwasaidia
wawekezaji wazawa kupata mikopo katika benki mbambali ili wawekeze zaidi
wananchi wapate ajira
Rais Magufuli alisema wawekezaji wazawa
katika viwanda viwili alivyovifungua mkoani Shinyanga wameonesha
uzalendo wa kweli kwa nchi yao na kuwataka watanzania kutoogopa
kuanzisha viwanda hata kama vingekuwa vidogo namna gani
Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainab Telack akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
na Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ambaye
pia ni mwenyekiti wa ALAT taifa wakimsikiliza rais Magufuli
Wa kwanza kulia ni mbunge wa Jimbo la
Shinyanga Mjini Stephen Masele akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Shinyanga Erasto Kwilasa na mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food
Products Company Limited Salum Mbuzi wakifuatilia hotuba ya rais
Magufuli
Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa
Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa na askari polisi wakati rais
Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food Products Company
Limited
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa wananchi zilizozalishwa katika
kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kilichopo katika
manispaa ya Shinyanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wakati akigawa soda
kwa wananchi zilizozalishwa katika kiwanda cha Jambo Food Products
Company Limited
Rais Magufuli akiendelea kugawa soda kwa wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa viongozi mbalimbali wa mkoa wa
Shinyanga wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kugawa soda
Rais Magufuli akiendelea kugawa soda
Rais Magufuli akigawa soda kwa kikundi cha wacheza ngoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akifungua soda kutoka katika kiwanda cha Jambo
Food Products Company Limited
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akinywa soda kutoka katika kiwanda cha Jambo
Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga-Picha na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia utamu wa soda kutoka katika kiwanda
cha Jambo Food Products Company Limited
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akionesha soda kutoka katika kiwanda cha Jambo
Food Products Company Limited
Wananchi wakiwa wamesimama baada ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuondoka
katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited baada ya kufungua
kiwanda hicho
Picha zote na Kadama Malunde
Hakuna maoni: