Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika katika ofisi ya Ruto, amenunua helikopta hiyo aiba ya Airbus H145, huku ikikamilisha taratibu na kwamba itawasili nchini Juni.
Ruto atakuwa mtu binafsi mwenye kumiliki helikopta inayoweza kufanya shughuli zake hata nyakati za usiku. Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) na polisi ndiyo yenye helikopta zenye uwezo huo.
Kwa mujibu wa jarida la Business Jet Traveler, helikopta hiyo mpya imegharimu Dola 9.7 milioni za Marekani (Sh970 milioni za Kenya).
Inaelezwa kuwa inaweza kutembea kilomita 480 kwa saa na ina uwezo wa kubeba abiria wanane.
Wanasiasa wanaomiliki helikopta
Wanasiasa wakiwamo viongozi wa vyama, magavana, maseneta, wabunge na wanaelezwa kuhitaji helikopta za kisasa.
Katika miaka miwili iliyopita, Rais Uhuru Kenya, Kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Peter Kenneth walielezwa kuwa waliomba kununua helikopta.
Hakuna maoni: