Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » MAZISHI YA MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU ALIYEUAWA KINYAMA SHINYANGA

Safari ya mwisho ya mtoto Happiness Kashinje mwenye umri wa miaka 9 aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni jeneza lililobeba mwili wa marehemu wakati wa shughuli za mazishi yaliyofanyika leo mchana katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na walimu na wanafunzi wa shule  aliyokuwa anasaoma mtoto huyo,wakazi wa eneo hilo pamoja na maeneo ya jirani,wadau wa haki za watoto,waandishi wa habari,mkuu wa intelijensia mkoa wa Shinyanga,viongozi wa dini na siasa wakiongozwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila.

Mtoto Happiness Kashinje enzi za uhai wake
 Shughuli za mazishi zikiendelea.Mtoto Hapiness Kashinje alikuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga na alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa  macho Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Wananchi wenye mapenzi mema wakiwa eneo la makaburini leo
Wanafunzi wa  shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga wakishiriki shughuli za mazishi ya mwanafunzi mwenzao aliyeuawa kinyama
 Walimu wa shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga wakishiriki shughuli za mazishi ya mwanafunzi wao
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akishiriki mazishi ya Happiness Kashinje leo mchana
Mazishi yanaendelea
Wananchi wakifuatilia shughuli za mazishi
Waandishi wa habari kulia wakiwa eneo alikozikwa mtoto Happiness
Wanafunzi wa shule ya msingi Negezi wakiwa eneo alikozikwa mwanafunzi mwenzao
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila (aliyeshikilia kofia) akizungumza baada ya mazishi ambapo alilaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.
“Kifo cha mtoto huyu ni mapenzi ya mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la hili lifuatiliwe hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinatishia amani Shinyanga”,aliongeza Nkulila.

 Mkuu wa  Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige (mwenye nguo nyeusi) akizungumza baada ya mazishi ambapo alisema suala la ulinzi kwa watoto ni jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.
“Hawa wahalifu wako katika jamii,mnawafahamu,toeni taarifa kwa jamii,wafichueni sheria ichukue mkondo wake”,aliongeza.
 Mkuu wa  Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige (mwenye nguo nyeusi)
 Akina mama wakiwa katika hali ya huzuni
Wainjilisti walioongoza ibada ya mazishi ya mtoto Happiness wakiwa mbele  kaburi la mtoto huyo baada ya mazishi
Baba mzazi wa mtoto Happiness Kashinje bwana Kashinje Mayala akizungumza na malunde1 blog baada ya mazishi ya mtoto wake kipenzi kuhusu tukio hilo ambapo alisema mwanaye alikuwa anaishi na shangazi  yake Mahegi Mayala na aliaga kwenda kunyoa nywele saluni majira ya saa tisa alasiri siku ya Jumapili na baada ya hapo hakurudi tena nyumbani.
Mayala alisema siku ya Jumatatu walipata taarifa kuwa kuna mtoto ametupwa kwenye vichaka karibu na Shamba la Mwandu Misona na walipofika eneo la tukio hawakumkuta mtoto huyo na kudaiwa kuwa amepelekwa na wasamaria wema katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Alisema kufuatia taarifa hizo aliamua kuufuatilia mwili huo hospitalini hapo ,ili kuweza kubaini kama ni mtoto wake na alipofika katika chumba cha kuhifadhia maiti alibaini mwili huo kuwa ni wa mtoto wake Happiness Kashinje.

Picha/Habari na Kadama Malunde-Shinyanga

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply