Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» » » AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMPIGA RISASI WAKITAKA UMAARUFU MTANDAONI AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMPIGA RISASI WAKITAKA UMAARUFU MTANDAONi

Mwanamke mmoja mjini Minesesotta nchini Marekani amehukumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake katika kile kinachosemekana ni mgogoro wa mtandaoni.
Monalisa Perez mwenye umri wa miaka 19 aliwekwa kizuizini baada ya kumpiga risasi Pedro Ruiz alipokuwa akishikilia kitabu katika kifua chake akidhani kitazuia risasi hiyo.
Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takriban watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YouTube alipompiga risasi mpenziwe.
Shangazie Ruiz anasema kuwa walifanya kitendo hicho ili kuimarisha ufuasi wao katika katika mitandao ya kijamii.
Claudia Ruiz aliiambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho '' kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi''. ''tunataka kuwa maarufu''.
''Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia'',''Musafanye hivyo''.
''Kwa nini utumie bunduki? Kwa nini?'', Claudia Ruiz aliambia chombo hicho cha habari.
''Walikuwa wakipendana sana'',alisema.''ulikuwa mzaha uliofanyika kimakosa''

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply