Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» » » Nay Wa Mitego Awachana Vibaya Young Killer, Barakah Da Prince

 

Nay wa Mitego
‘MDUNGUAJI’ bei mbaya kwenye kilinge cha Hi-hop, Emmanuel  Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amekoleza moto bifu lake na wasanii chakaramu, Baraka Andrew ‘Da Price’ na Young Killer, ambapo pamoja na mambo mengine, amefafanua kwa kina mistari aliyowaimba kenywe wimbo wake mpya wa Moto.

Katika mahojiano maalum na Global TV Online, Nay au The True Boy ameweka wazi bila kutafuna maneno, kuwa Young Killer na Baraka  wamepoteza mweleko kwenye ramani ya muziki na kwamba kuna mahali walikosea, hivyo wajirekebishe vinginevyo watarudi Mwanza kuvua samakiBarakah

Katika kuonesha amedhamiria kuwawashia moto, prezidaa huyo wa lebo ya Free Nation, amesema Da Prince arudi ampigie magoti prodyuza Kid Bway, kwani ndiye alimuonesha mwanga wa muziki lakini malipo ya dogo ni dharau na mateke ya punda, ndiyo chanzo cha kuporomoka kwake kimuziki.Young Killer

Kuhusu Young Killer, Nay alisema ni lazima amuangukie Mona Ganstar kwani amemtoa kikazi, lakini amemlipa matusi na dharau. Nay amesema watu hao ‘wamekunja’ hivyo ni ngumu kwa wasanii hao kufika mbali kimuziki. Huku akiwakumbusha kuwa na nidhamu, kuandika mashairi na kuimba havitoshi.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply