Siku moja tu baada ya mtandao huu kuripoti kuhusu tukio la mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda manispaa ya Shinyanga Jacob Paul kujiua kwa kujinyonga leo tunayo habari nyingine ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Sada Elias (24) mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga ambaye amefariki dunia baada ya kujichinja kwa kisu kisha kupasua chupa ya soda na kujichoma nayo kwenye koromeo.Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde anaripoti.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
wanasema mwanamke huyo aliyekuwa anaishi na mwanae wa miaka mine na
mdogo wake aliyejulikana kwa moja la Vesi (12) alichukua uamuzi wa
kujiua usiku wa kuamkia Juni 8,2017 majira ya saa nane usiku.
Akielezea kuhusu tukio hilo jirani/mpangaji mwenzake na marehemu,Peter
Maduhu alisema siku ya tukio majira ya saa nane usiku,mdogo wake na
marehemu aitwaye Vesi alipiga kelele akitoka ndani ya chumba wakichokuwa
wanaishi akidai dada yake anajiua kwa kisu.
“Wakati anatoka ndani alikuwa tayari amemunyang’anya kisu, tuliamka
kwenda katika chumba hicho lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa
ndani,tukaamua kuvunja mlango tukakuta amevunja chupa akijichoma nayo
kwenye koromeo,polisi walivyokuja tukampeleka hospitali kwa ajili ya
matibabu”,alieleza Maduhu.
Alisema Sada Elias alifariki dunia siku ya Ijumaa majira ya saa tano
usiku wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Shinyanga.
Maduhu alisema kabla ya kifo chake,jirani yake huyo ambaye alikuwa
anajishughulika na shughuli ya kuuza chakula “Mama Ntilie” alikuwa
analalamika kuumwa kwa muda mrefu bila kutaja ugonjwa uliokuwa
unamsumbua.
Akisimulia kuhusu tukio hilo baada ya mazishi yaliyofanyika leo Jumapili
Juni 11,2017 mchana,Mwenyekiti wa mtaa wa Mabambasi David
Nkulila,ambaye pia ni diwani wa kata ya Ndembezi,alisema kifo cha
mwanamke huyo kinatokana na msongo wa mawazo.
“Huenda kifo hiki kimetokana na msongo wa mawazo,alikuwa anaishi peke
yake na watoto hao wawili,pengine kutokana na ugumu wa maisha na alikuwa
analalamika anaumwa,aliamua kujifungia ndani ya chumba chake huku
akiwaambia watoto wake kuwa mtu yeyote atakayeuliza kuwa kaenda
wapi,wamwambie yupo kazini”,alieleza Nkulila.
Nkulila aliwataka wananchi pindi wanapopata matatizo wasinyamaze kimya
bali waombe ushauri kwa watu wanaowazunguka ikiwemo wazee na viongozi wa
dini na kuhakikisha wanamshirikisha mwenyezi Mungu.
Naye baba wa marehemu Elias Luleju mkazi wa kata ya Nyakahula wilaya ya
Biharamulo mkoani Kagera aliushukuru uongozi wa mtaa huo kwa ushirikiano
waliouonesha wakati wa msiba huo na aliamua kuwachukua watoto aliokuwa
anaishi nao marehemu huku akidai mume wa mwanaye yuko wapi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amethitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amethitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mwili wa marehemu Sada Elias ukiwa umetolewa kwenye msikiti wa Masjid
Aqswa Ngokolo A (gari la upande wa kulia) leo majira ya saa saba mchana
Mwili wa marehemu Sada Elias ukishushwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi katika makaburi ya Mshikamano Ngokolo mjini Shinyanga
Wananchi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu
Mwenyekiti wa mtaa wa Mabambasi David Nkulila,ambaye pia ni diwani wa
kata ya Ndembezi akizungumza baada ya mazishi ya marehemu Sada Elias
Baba wa marehemu Sada mzee Elias Luleju mkazi wa kata ya Nyakahula
wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akiwashukuru wananchi wa mtaa wa
Mabambasi kata ya Ndembezi kwa ushirikiano waliompa wakati wa msiba huo
kwani yeye anaishi Kagera amefika mtaani hapo kwa ajili ya mazishi na
kuchukua watoto waliokuwa wanaishi na marehemu.TUTUMIE HABARI KUPITIA- 0763288300
Hakuna maoni: