Dola za Marekani
Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika
kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikiendi iliyopita kulingana na chombo
cha habari cha taifa.
Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua ,nduguze
walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo
hatozikwa.
Nduguze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuyafikia majukumu yake
ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga
hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika
kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya
dola 800 na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha
dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha
zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa,walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Mozambique
hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia
utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Hakuna maoni: