Pambana kwa kila hali, mpaka utoke kwenye chanagamoto za kimaisha. |
Ninasema inakuwa haisaidii kwa sababu, unakuwa bado upo pale pale kwenye changamoto zako, na dawa pekee ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kutoka kwenye changamoto hiyo kwa namna yoyote ile.
Haijalishi unapita kwenye kipindi gani, lakini lilokubwa kwako ambalo kila wakati unapaswa kulielewa na kuliangalia zaidi ni kwa jinsi gani wewe utaweza kumudu hali hiyo ya kutokata tamaa na kuendelea na maisha yako unapokuwa kwenye kipindi hichi.
Ni lengo la makala haya, kukupa mwanga na kukuonyesha njia ya kupita, ili ikusaidie kutokukata tamaa, wakati unakutana na changamoto kubwa za kimaisha. Hapa inabidi uwe shujaa upigane mwanzo mwisho.
Unawezaje kutokukata tamaa katika kipindi kigumu unachopitia nyakati mgumu za maisha? Yafuatayo ni mambo ya msingi kuzingatia ili usikate tamaa katika kipindi ambacho unakutana na changamoto ngumu katika maisha yako.
1. Kipindi cha nyakati ngumu, siyo chako peke yako.
Nyakati ngumu unazopitia au changamoto unazopitia, kitu cha kwaza ambacho unatakiwa uelewe, wewe sio mtu wa kwanza kukutana nazo, bali wapo watu ambao wameshakutana nazo sana na wakaishinda pia.
Kama hiyo ilitokea kwao hivyo, basi hata wewe unayo nafasi ya kuishinda changamoto hiyo na kuwa mshindi kwenye maisha yako. Huna haja ya kujuta au kuendelea kulia sana, jipe moyo na utashinda majaribu hayo.
2. Nyakati ngumu katika maisha, zinakujengea ukomavu.
Maisha yanajengwa kwa namna tofauti. Kipo kipindi yanaweza kujengwa katika njia ya kawaida na kuna wakati yanajengwa kwenye njia ngumu na hatari kama hiyo ya changamoto na nyakati ngumu.
Ukilijua hilo, basi elewa unakomazwa na maisha. Siku ukija kutoka hapo utakuwa kama dhahabu ambayo tayari imeshapitia kwenye moto. Utakuwa umekamilika kila eneo na hakuna kitakachokubabaisha.
3. Nyakati ngumu katika maisha, zinakusaidia kukujengea hali ya uvumilivu mkubwa sana.
Sio siri tena, unapopitia katika nyakati ngumu katika maisha yako, ni kipindi ambacho unapitia kwenye uvumilivu mkubwa sana. ukilielewa hili, itakusaidia sana kupita kwenye nyakati zozote ngumu zinazojitokeza kwenye maisha yako hata kwa baadae.
Kwa kuzingatia mambo hayo, bila shaka utakuwa umepata mwanga ni kwa jinsi gani unaweza ukapita kati kati ya nyakati ngumu zinazoweza kujitokeza katika maisha yako wakati wowote na ukawa mshindi mkubwa.
Chukua hatua katika kufikia mafanikio makubwa na pia endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kwa kuweza kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Hakuna maoni: