Ovyooo! Msichana wa mjini asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias
Semagongo ‘Aunty Lulu’, kwa mara nyingine amefanya kituko cha aina yake
baada ya kuzua timbwili kisha kusaula nguo zote hadharani bila kujali
yupo ukweni.
Aunty Lulu ana uhusiano wa kimapenzi na kijana anayejulikana kwa jina moja la Amani.
Habari zisizokuwa na chembe ya ‘dauti’ zilidai kuwa hivi karibuni, Aunty
Lulu na Amani walikuwa wakipata kinywaji kwenye baa moja iliyopo jirani
na nyumbani kwa wakwe zake maeneo ya Majohe, Dar ndipo ukaibuka ugomvi
kati yao na kusababisha pachimbike.
Chanzo hicho kutoka ndani ya familia ya wakwe zake Aunty Lulu,
kilidai kwamba mwanadada huyo alizua timbwili alipokuwa akipigana na
Amani.
Ilisemekana kwamba katika hali ya kushangaza, Aunty Lulu alikwenda
mbali zaidi alipovua nguo hadharani na kubaki mtupu hivyo kuwalazimu
watu wenye busara kumshika na kumsihi avae nguo kisha walimpeleka
nyumbani wanakoishi maeneo hayohayo ya jirani na wakwe zake.
“Yaani Aunty Lulu anamng’ang’ania kwa nguvu ndugu yetu Amani wakati
familia nzima haimtaki kwa sababu ya tabia zake hizo, hii ni mara ya
pili kuvua nguo hadharani.
“Ukweli hata baba mkwe hataki kumsikia, ameshampigia sana kelele mwanaye aachane naye,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika
kwa kuanzia na Aunty Lulu ambapo alikiri kwamba ni kweli ugomvi ulitokea
lakini hakuvua nguo.
“Ni kweli tuligombana hapo baa
lakini sikuvua nguo na kuhusu kila siku kupigana, jamani hayo ndiyo
mapenzi. Wanaosema mimi ndiye namng’ang’ania Amani siyo kweli kwani wote
tunapendana,” alisema Aunty Lulu.
Kwa upande wake Amani alifunguka: “Habari hizo siyo za kweli kabisa ndugu mwandishi.”
Home
»
»Unlabelled
» Aunty Lulu Avua Nguo Hadharani Ukweni
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: