ISHARA za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb
amekula kichapo na kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika
nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na dogo wa kiume aliyedaiwa kuwa
ni denti wa sekondari.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb akiwa amepigw pingu baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kiume gesti.
Aibu hiyo ya karne ilijiri juzi Jumatatu kwenye gesti hiyo (jina
linahifadhiwa) iliyopo maeneo ya Manzese, Dar ambapo jamaa huyo alikutwa
chumbani na denti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoitonya Timu ya Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) ya Global Publishers, njemba huyo amekuwa na ‘katabia
kachafu kakuwafanyia usodoma’ watoto wa kiume.Habari hizo zilidai kuwa
ishu hiyo iliwakera wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimfuatilia kwa muda
mrefu ndipo wakaamua kumfungia kazi baada ya kudaiwa kuwa na mtoto huyo
chumbani usiku kucha.
Kwa mujibu wa meneja wa gesti hiyo (aligoma kuta jina) ambaye alitoa
ushirikiano wa kutosha kwa OFM, raia hao walikuwa wakimchunguza njemba
huyo kwa muda mrefu kutokana na tabia ya kulala kwenye gesti hiyo na
watoto wa kiume.
Njemba aliyekutwa na denti akipanda kwenye difenda.
“Mwanzo tulifikiri anakuja na vijana hao kama marafiki zake wa
kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa alikuwa
akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo
alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa
chumba kama kawaida.
“Wahudumu waliniambia kuwa jamaa
amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini safari hii alifika peke
yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake kwani siyo kawaida yake
so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu
walisikia miguno ndani ya chumba alicholala njemba huyo ndipo
wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na vijana wa OFM ambao walifika
eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’.
Meneja huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo
muda gani kwani walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na
machale.
Hata hivyo, Jiji la Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo
walijazana kwenye gesti hiyo kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi
walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na kuwampeleka Kituo cha Polisi cha
Magomeni, Dar.
Hadi OFM inang’oa nanga kituoni hapo, njemba huyo na
kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea kuhojiwa. Kujua kilichojiri
usikose kufuatilia magazeti ya Global.
Home
»
»Unlabelled
» Aibu! Njemba anaswa na Denti wa kiume GESTI
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: