TAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha
ambaye aliwahi kutangaza kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta
akiumbuka kwa mashabiki wake kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu
kwa kuachia kazi mpya na kuandaa matamasha mbali mbali.
Msanii huyo alitoa uamuzi huo kwa madai kuwa alichoshwa na skendo za
kila kukicha ambazo wakati mwingine zimekuwa zikimshushia hadhi katika
jamii, ikiwemo skendo ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.
Hakuna maoni: