Tapeli
Sugu aliyejulikana kwa Jina la Ally Mwinyi Kutoka Vikindu-Pwani
aliyekamatwa Parking za Madereva wa Wabunge-Dodoma akiwa chini ya Ulinzi
tayari kwa Kupelekwa Kituo cha Polisi kwa hatua za Kisheria.
Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mwinyi na
Kujitambulisha anatokea VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi la polisi kwa
Ushirikiano na Madreva wa Wabunge hapa Dodoma kwa tabia yake Mbaya ya
Kutapeli watu.
Kijana huyo amekuwa akijihusisha na Matukio Mbalimbali ya
Utapeli hapa Dodoma kwa nyakati tofauti na kwanji tofauti na kwa watu
tofauti.Utapeli wake amekua akiufanya kwenye Uuzaji wa Viwanja akijidai
yeye ni Dalali wa Viwanja,Pia amekamatwa akiwa na Fungo “FAKE” za Gari
ambazo amekuwa akitumia kutembea nazo na kujidai yeye ni Dreva wa TASAF
amekwama Dodoma hivyo anahitaji Msaada,Kwa nyakati tofauti Madreva
wamekuwa wakikutana naye na kuwaomba masaada na hatimaye Kupewa fedha za
Kumuwezesha Kurudi Dsm alikosema ndio anafanya kazi ya TASAF.
Lakini hadi jana anakamatwa akiwa kwenye jaribio la Kumtapeli
Dreva wa Mh:Makongoro Mahanga, ameshadanganya Madreva Wengi na bado
amekuwa akionekana Dodoma tofauti na maelezo yake kuwa anahitaji msaada
wa Nauli arejee Dsm tangu Bunge la Katiba Kuanza,Pia ameshukiwa
kutapeli watu wengi fedha likiwamo jaribio la Kuiba pikipiki eneo la
Kituo cha Polisi Dodoma.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Rai,Kama Umetapeliwa Dodoma,tafadhali fika Kituo cha Polisi Dodoma Mjini kwa msaada zaidi.
Hakuna maoni: