Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » KAHAMAYETU:Mwanafunzi wa shule ya msingi abakwa,apoteza fahamu….

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Liami wilayani Ifakara mkoani Morogoro (jina limehifadhiwa), amebakwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Mei 5, mwaka huu nyumbani kwa bibi yake.

Akizungumza na gazeti hili, mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Neema Ally akiwa wodi A ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema mtoto wao alienda nyumbani kwa bibi yake kulala baada ya kumaliza kula kwa wazazi wake.

Alisema watu waliofanya unyama huo, pia waliiba baiskeli kabla ya mtoto wao kuokolewa na wasamaria wema waliosikia mayowe yake ya kuomba msaada ambapo walimkuta akitokwa na povu mdomoni.

dentMwanafunzi ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa hoi hospitali baada ya kubakwa.

Alisema wasamaria wema hao walimkuta mtoto wake akiwa amepoteza fahamu kutokana na kukabwa koo wakati akifanyiwa kitendo hicho.

“Hali ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa Hospitali ya St. Frances, Ifakara ambako nako hakukaa, akahamishiwa hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
dent2Mama wa mtoto huyo akiwa na binti yake hospitalini.


“Ilimchukua muda wa siku tatu mtoto kupata fahamu, nawashukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara kwa  kutoa  gari la kubebea wagonjwa kwa haraka ili kunusuru maisha ya mwanangu na fedha,” alisema Neema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply