Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » KAHAMAYETU:MTEJA WAKE HUKO GEITA MGANGA WA KIENYEJI ACHINJWA KIKATILI BAADA YA KUCHUKULIWA NA MTEJA WAKE HUKO GEITA


Mwanamke Mwamvua Salum Maarufa mama Rembe (48) ameuawa Wilayani Bukombe Mkoani Geita kwa kuchinjwa na watu ambao hawakujulikana ambapo mwili wake umekutwa katika nyumba moja ambayo haina watu wanaoishi.

Mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Ipulwa kata ya ushirombo wilayani bukombe mkoani geita.
 
Mume wa marehemu huyo ramadhani Pembela amedai mke wake alipata mkasa huo wakati yeye hayupo alikwenda kulala kwa mke mkubwa kabla ya kujulishwa kuwa mke wake ameuwawa.

Marehemu mama Lembe alikuwa mganga wa jadi, habari zaidi kutokandani ya familia zinadai kuwa mama huyo aliondoka juzi saa mbili usiku kwenda kutoa huduma wakati akiwa amefuatwa na mtu mmoja akatoe huduma.

Lakini mauti hayo yamemkuta mama huyo ambaye alionekana akiwa amechijwa katika jumba bovu na mazishi yake yamefanyika jana wilayani bukombe

Jeshi la polisi wilayani Bukombe limethibitisha kutokea kwa tukio hilo hivyo upelelezi wa mauaji hayo unaendelea ili watakao bainika wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hiyo.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply