UMOJA WA
WAFANYAUSAFI WA MAZINGIRA KAHAMA WAILALAMIKIA HALMASHAURI YA MJI KUWAFANYISHA
KAZI BILA MKATABA
UMOJA wa
wafanya usafi wa mazingira katika
halmashuri ya mji wa kahama mkoani shinyanga wameulalamikia uongozi wa Afya
katika Halmashauri hiyo kwa kuwafanyisha kazi bila Mkataba wowote kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Baadhi ya wafanya
usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya mji huo juu ya utaratibu wa kufanya kazi kama waajiriwa au wanafanya kazi kwa mkataba.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wafanya usafi barabarani,maziku John alisema kuwa wanafanya kazi
bila ya Mkataba wowote hali ambayo inapelekea kwa Baadhi ya Wafanyakazi
kuachishwa kazi bila utaratibu wowote kitu ambacho ni tofauti na sheria ya
Utumishi.
John
aliendelea kusema kuwa halmashauri ya Mji inawalipa mshahara wa Shilingi laki
moja kama Vibarua kwa kila mwezi kwa kuwapa mkononi ambapo alidai kuwa fedha
hiyo haikidhi hata mahitaji yao ya kila siku.
Hata hivyo
Wafanya usafi hao wakiongea na nipashe kwa nyakati tofauti walieleza kuwa pamoja na
Halmashauri hiyo kuwalipa mshahara yao walisema endapo mfanyakazi ameugua
anajigharamikia mwenyewe na kipindi wanapoenda Hospitalini kwa matibabu
hawatambuliki kama wafanyakazi na kuelezwa kuwa si waajiriwa.
Kutokana na
kufanya kazi pasipo na mkataba wowote imepelekea kwa baadhi ya wafanyakazi
kufukuzwa holela na Afisa huyo wa Afya Masele
katika sehemu yao ya kazi bila utaratibu wowote na kuweka wengine hali
waliyodai kuwa huenda Rushwa imetendeka.
John
aliwataja baadhi ya wafagiaji wa
Barabara za Mji huo kuwa ni pamoja na
Tatu Khamisi, Obed Samsoni,Eliyanzima Sehemu na Lucia Mabala ambapo alisema kuwa niwazoefu wa kazi hizo
kwa miaka mingi tangu enzi za Halmashauri ya Wilaya.
Kwa upande
wake Afisa Afya wa Mji ,Martini Masele,Mtanzania ilipomtafuta kwa njia ya simu
yake ya kiganjani baada ya kumkosa Ofisini kwake alipokea simu alipohojiwa
kuhusiana na malalamiko hayo alikata simu na kuifunga
Hakuna maoni: