CHAMA cha
Mapinduzi Mkoa Shinyanga kimewataka Wabunge
katika mchakato wa kupata Katiba Mpya Jamhuri ya Muungano kuhakikisha
kuwa wanarudisha Madaraka kwa Wananchi kwani suala la Serikali tatu lipo ndani
ya Serikali mbili kupitia Serikali za mitaa.
Hayo
yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati
akizungumza na wakazi wa Mji mdogo wa
Isaka katika moja ya kukagua ilani ya Chama hicho kama inatekelezwa.
Mgeja
aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania tayari inazo Serikali tatu ambazo hazina
gharama yeyote na kufafanua kuwa Serikali kwanza ni ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya tatu ni Serikali za Mitaa.
Alisema kuwa
Mfumo ulipo sasa ni wa Serikali tatu ndani ya Mfumo wa Serikali mbili na
kuongeza kuwa mfumo huo ni mzuri ambao hauna gharama na mzigo mkubwa kwa Wananchi wa Tanzania.
Mwenyekiti
huyo aliwaomba Wabunge wa Bunge la Katiba pamoja na Watanzania wote kutambua
kuwa Serikali ya tatu ipo nayo si Serikali za mitaa ambayo ni Serikali ya
Demokrasia na yenye mamlaka kamili kwa Wananchi ambao wamejiamulia wenyewe na
kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo husika.
“Ninawaomba
Watanzania kuwa na Serikali za Mitaa ni jambo la kujivunia kwa kuwa wananchi
watakuwa wakijiongoza wenyewe kupitia mabaraza yao ya Madiwani”, Alisema
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Hata hivyo
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kupitia Mabaraza ya Madiwani kwa sasa
wananchi wameweza kufaidika na mambo mengi katika sekta mbalimbali za huduma za
kijamii zikiwemo sekta za maji, Afya Elimu, Barabara, Kilimo, uvuvi, Ufugaji na
Utamaduni.
Alisema kuwa
mambo yote yanayofanyika kwa sasa kupitia Serikali kuu baadhi ya mambo na majukumu yanaweza kufanywa
kupitia Serikali za Mitaa kwa kuwa mfumo ni uleule unatumiwa na kuwataka
Wabunge wa Katiba kufikiria kwa makini juu ya mchakato huo unaoendelea ili
kuwapa mamlaka kamili wananchi kuliko kuwatwisha mzigo mwingine wa Serikali tatu wa kuendelea kutawaliwa.
Aliendelea
kusema kuwa kuwepo kwa Serikali za mitaa kunatosha kujibu kiu ya watu
wanaolilia kuwepo kwa Serikali tatu na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa wakati huu amewashauri wabunge wa Katiba wote bila ya kujali itikadi zao za
Vyama na makundi ya uwakilishi kuunga mkono mawazo hayo yenye manufaa kwa
Wananchi na Taifa kwa ujmla.
“Kuwepo kwa
Serikali za mitaa kunatosha kujibu kiu ya watu wanaolilia kuwepo kwa Serikali
tatu na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa
wakati huu amewashauri wabunge wa Katiba wote bila ya kujali itikadi zao za
Vyama na makundi ya uwakilishi kuunga mkono mawazo hayo yenye manufaa kwa
Wananchi na Taifa kwa ujmla”,Alisema Mgeja
Hakuna maoni: