Mkuu wa wilaya ya kahama
Benson Mpesya Akiwa na Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya Afrrican
Barrick Gold Mine Brad Gordon mwenye kitambulisho cheupe wakati wa
ukanguzi wa barabara za mji wa kahama Ambao umefadhiliwa na Mgodi wa
Buzwangi kwa kiwango cha Lami kwa Gharama ya bilioni 3
Mkuu wa wilaya ya kahama
Benson Mpesya ambaye anaonyesha mkono Mkurungezi Mtendaji wa kampuni
ya Afrrican Barrick Gold Mine Brad Gord ujenzi wa Barabara ya Lami Mjini
kahama (ABG)
Mmoja ya mitaa ya mji wa kahama Ambayo ipo katika kiwango cha lami huu ni moja wa mtaa wa igalilimi
Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Buzwangi Moses Msofe mwenye shati nyeupe Akimsikiliza mkuu wa wa wilaya kahama.
Mkuu wa wilaya ya kahama
Benson Mpesya mwenye suti nyeusi wa kati Mkurungezi Mtendaji wa kampuni
ya Afrrican Gold Brad Gordon mwisho kulia ni Meneja wa Mgodi wa
Buzwangi Philiber Rweyemamu na nyuma ni jamal Rwambo mwenye shati la
mistali .
Mmoja ya mifereji ambayo ipo kati kati ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami mjini kahama
Mkuu wa wilaya kahama Benson Mpesya Akiongea na Waandishi wa habari Hawapo pichani
Mkuu wa wilaya kahama
Benson Mpesya Akiwa na Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya Afrricani
Barrick Gold Mine Wakiwa ofisi kwake leo kwa ajili ya kuona Mradi wa
barabara za mji wa kahama kwa kiwango cha Lami ambao ujenzi huu
hutachukuwa muda wa miezi 6
MKuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya Akisisitiza jambo leo na uongozi wa Afrrican Barrick Gold mine Hawapo pichana
Mmoja ya Barabara za Mji wa mji wa Kahama Ambazo zilivyo sasa baada ya kuwekewa Lami
Mkurungezi Mtendaji wa
Afrrican Barrick Gold Mine Brad Gordon Mwenye Kuonyesha ubora wa
Barabara jinsi zilivyojengwa kwa kiwango cha Lami mwenye Tsheti ya Blue
ni Meneja wa Mgodi wa Buzwangi Philiber Rweyemamu .na mwenye shati jeupe
ni muandishi wa habari wakipokea maelenzo
Mkurungezi
Mtendaji wa Afrrican Barrick Gold mine Brad Gordon na Meneja wa Mgodi
wa Buzwangi Philiber Rwayemamu picha zote na Mohab Dominick
KAMPUNI
ya ya African Barrick Gold Mine inayomiliki Migodi ya dahabu ya
Bulyanhulu na Buzwagi imetumia jumla ya Shilingi Bilioni 64 katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii kwa jamii inayozunguka Migodi
hiyo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Brad Gordon alisema Kampuni yake imetumia
fedha hizo katika kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi
wanayozunguka Migodi hiyo katika sekta mbalimbali za Elimu, Afya, Maji
pamoja Michezo kwa lengo la kuharakisha maendeleo na ustawi wa jamii.
Hayo
aliyasema wakati wa ukaguzi wa barabara zanye urefu wa zaidi ya
Kilometa sita zinazojengwa kwenye mji wa Kahama kwa kupitia ufadhili wa
Kampuni hiyo ya African Barrick Gold kwa kushirikiana na Serikali kwa
lengo la kupunguza adha ya vumbi na ubovu wa barabara zilizokuwepo
awali.
Alisema
kampuni hiyo imeamua kushirikiana na serikali kujenga miundombinu hiyo
ili kuiwezesha jamii kuwa karibu na migodi yake na kuondoa dhana
iliyokuwa imezoeleka kuwa wawekezaji hawanafaida yoyote kwa wananchi na
kuwa itaendelea kutengeneza miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo
ili kuharakisha maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema mji wa
Kahama unakuwa kwa kasi kutokana na shughuli za madini zinazofanywa na
migodi hiyo miwili mikubwa ya Bulyanhulu na Buzwagi na hivyo inahitaji
mipango ya haraka kuuwezesha kuwa na miundombinu muhimu kama vile
barabara za lami, taa, na mifumo mizuri ya kutiririsha majitaka.
Alisema
serikali inatambuaumuhimu wa uwepo wa wawekezaji katika kusaidia
shughuli muhimu za maendeleo na hivyo kuitaka jamii kushirikiana nao
badala ya kuwabeza hawarudishi faida wanayoipata kwa ajili ya maendeleo
yao.
Aliongeza
kuwa serikali itahakikisha inasimamia sera yake ya uwekezaji na
kuwahakikishia usalama wawekezaji hao ili wafanye kazi zao kwa amani na
utulivu kwa lengo la kusogeza mbele gurudumu la maendeleo ya taifa.
Kampuni
ya African Barrick Gold (ABG) imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 3.2
kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo za kiwango cha lami zinazozunguka
mji wa Kahama huku mchango wa serikali katika ujenzi wake ikiwa ni
shilingi Milioni 700 kutoka ofisi ya waziri mkuu.
Hakuna maoni: