KATIKA
hali ya kushangaza iliyojitokeza kwa Jeshi la Zimamoto la Halmashauri ya Mji wa
Kahama ni pale ambapo wamekosa ofisi ya kufanyia kazi na kuhamishia katika eneo
ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na makaburi hapo awali.
Jeshi
hilo ambalo ni muhimu katika matika matukio ya uzimaji wa moto katika Mji wa
Kahama pia wamejikutaa wakikosa ofisi za kufanyia kazi hali ambayo imewafanya
kufanyia shughuli zao za kiofisi katika gari lao la kuzimia moto.
Baadhi
ya watumishi wa Jeshi hilo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuhsu kupatiwa
eneo la kufanyia kazi lakini jitihada zao zimekuwa zikigonga mwamba bila ya
mafanikio huku wakiendelea kusota katika mazingira magumu ya kufanyia kazi
Akiongea
na Habarileo juzi Mkaguzi wa Jeshi hilo
Mkoa wa Shinyanga Rashidi Mwinyimkuu alisema kuwa madai hayo yanayodaiwa na
Askari wa jeshi ni ya msingi na kungeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kupata eneo
la kufanyia kazi lakini mazungumzo bado yanaendeleo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Msalala.
“Unajua
ndugu Mwandishi Jeshi la zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Kahama
limeanzishwa hivi karibuni baada ya kuzaliwa kwa Halmashari hiyo na kwa sasa
tupo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunapata maeneo kwa ajili ya
kufanyia kazi Ashari hawa”, Alisema Rashidi Mwinyimkuu.
Pia
Mkaguzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa Wananchi wa Mji wa Kahama
wanahitaji kupata elimu kubwa juu ya matukio yanayohusu moto ikiwa ni sambamba
na kutumia vifaa maalumu vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya maduka
mahotel na sehemu nyingine.
Aliendelea
kusema kuwa Wilaya ya Kahama kwa sasa inakuwa kwa haraka zaidi na watu
wakiendelea kujenga nyumba nyingi ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara kuwa
mengi hali ambayo kwa kuwa na ofisi ya zimamoto katikati ya mji itasadia wa
kiasi kikubwa kuwahi matukio.
Hata
hivyo Mkaguzi huyo alisema kuwa Changamoto nyingine inayoikabili ofisi yake ya
zimamoto ni pamoja na kutokuwa na namba maalumu kwa ajili ya Wananchi kupiga
pindi matukio ya moto yanapotokea na kungeza kuwa hali hiyo inatokana na
kutokuwa na ofisi maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi.
Hakuna maoni: