Hizi
ni taarifa zingine za ghafla ambazo Tanzania tumezipokea kwa mshtuko
na masikitiko ni kifo cha miongoni mwa-madirector wa Tanzania ambao ni
waigizaji pia,huyu ni Adam Kuambiana ambaye taarifa za kifo chake
zimeanza kusambaa mchana wa Mei 17.
Marehemu Adam Kuambiana akiwa location enzi za uhai wake.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema>>’Mwenzetu Adam Philipo
Kuambiana amefariki akiwa Location ana shoot,mimi nimepigiwa simu saa 3
asubuhi kuwa hospitali pale Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli
Adam amefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam Kuambiana amefariki’
‘Sasa
hivi tumetoka Muhumbili kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema
wakati yupo location alikua analalamika tumbo linamuuma linamuuma
kumfikisha hospitali ndipo umauti ukamfika’.
Kwa
mujibu wa Steve Nyerere amesema kuwa marehemu Adam kuambiana alikua
ana shoot filamu yake mpya ambayo ndani yake amewashirikisha wasanii
kadhaa wa Bongo fleva akiwemo Q Chillah,taratibu za mazishi na msiba
kwa ujumla endelea kufuatilia kahamamatukio.blogspot.com tukufahamisha kila kinachoendelea.
Hakuna maoni: