Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » AFARIKI DUNIA KWA KUANGUKIA KIFUSI MACHIMBONI MWIME KAHAMA

MTU mmoja amekufa dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya kufukiwa na Kifusi katika Shimo walilokuwa wakichimba Dhahabu kwenye Machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kijji cha Ilindi kata ya Zongomera Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Mkoani Shinyanga, Nicodemas Majaba alisema tukio hilo limetokea jana asubuhi majira ya saa nne ambapo Marehemu huyo alikuwa akichimba dhahabu na wenzake  mara ghafla wakashukiwa na kifusi kilichosababisha kutokea kwa mauaji hayo.
Majaba alimtaja aliyepoteza maisha katika tukio hilo ni Ezekieli Moshi (35) Mkazi wa kijiji cha Mhunze Wilaya ya  Bariadi mkoani Simiyu na wengine wawili  waliojeruhiwa ni Jacob Omoro(35) mkazi wa katoro pamoja na Njile Sospiter (30) mkazi wa bariadi.
Aidha katika hatua nyingine  Majaba alisema kuwa  mashimo hayo yaliyoleta maafa yalikuwa yamesimamishwa kufanya kazi mpaka hapo baaye yatakapotafutiwa  ufumbuzi.
Hata hivyo pamoja na majeruhi hao kulazwa Katika Hospitali  ya Wilaya ya Kahama Mkoani shinyanga Mganga Mfawidhi Joseph Fwoma alisema kuwa hajapata taarifa juu ya Majeruhi hao kulazwa katika hospitali hiyo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga  kihenya kihenya  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wachimbaji wachukue tahadhari na kuacha kuchimba dhahabu katika mashimo yasiyokuwa rasmi.
 mwisho

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply